Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemteua, Catherine Nyako Ruge kuwa mbunge wa viti maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha jana imemteua Ndugu Catherine Nyakao Ruge kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Dkt. Elly Marco Macha.

Tume ya hiyo imemteua Catherine Nyakao Ruge baada yakupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Spika alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwepo nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo baada ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Dkt. Elly Marko Macha kufariki dunia na hivyo kuwepo nafasi wazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *