Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina, Carlos Tevez amejiunga na klabu ya Shanghai Shenhua ya China akitokea klabu ya Bocca Junior ya Argentina.

Carlos Tevez atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni 615,000 kwa wiki ambao ni mkubwa kuliko anaolipwa mchezaji yeyote mwingine duniani.

Klabu hiyo inayonolewa na kocha Gus Poyet imeamua kujiimarisha kwa ajili ya ligi kuu nchini China ‘China Super League’ ambapo inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Guangzhou Evergrade.

carlos

Tevez ni mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Manchester United na Manchester City anajiunga na ligi kuu nchini China baada ya ligi hiyo kwasasa kuwa na mvuto wa kipesa mpaka kupelekea mastaa wengi kujiunga na klabu za uko.

Mbali na Tevez kutimkia China wengine waliojiunga na timu za China ni Oscar ambaye atajiunga mwakani kwenye klabu ya Shangha SIPG  pamoja na Ramirez anayechezea klabu ya Jiangsu Suning FC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *