Mwanamitindo maarufu nchini, Calisah amesema kuwa mwaka huu wa 2017 hakuna kazi iliyomuingizia kipato kikubwa kama tangazo la kuvaa viatu vya kike.

Calisah alizua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kurusha picha kwenye Instagram akiwa amevaa viatu vya kike.

Calisah amefunguka na kudai kuwa dili hilo alilipata kwa ajili ya kutangaza viatu vya kike Instagram kutoka kampuni Fulani na dili hilo lilimuingizia kiasi cha shilingi milioni saba za kitanzania.

Baada ya picha hizo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kila mtu aliongea lake na hata wapo waliodai kuwa Calisah atakuwa ni shoga kutokana na kuvaa viatu vya kike jambo alilokataa kwa nguvu zote na kusisitiza kuwa yeye ni rijali na wala sio shoga.

Lakini mwenyewe amekiri kuwa hakuna kazi iliyomuingizia kipato sana kwa mwaka 2017 kama suala la kutangaza viatu hivyo, pia mwanamitindo huyo amesema kuwa yupo tayari kuvaa hata gauni kwenye tangazo lakini alipwe mkwanja mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *