Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Bushoke amesema kuwa baada ya Papii Kocha kutoka jela kwa msamaha wa rais wanatarajia kuingia studio kurekodi wimbo wa pamoja.
Bushoke amesema amefurahi sana rafiki yake huyo kuwa huru huku akiahidi kuanza kufanya mchakato wa kumrudisha kwenye game rasmi baada ya kukosekana kwenye game ya muziki kwa kipindi cha miaka 13 baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.
Mwanamuziki huyo aliyewahi kufanya kazi na Papii Kocha kabla ya kufungwa amesema kuwa anataka kumrudisha rafiki yake kwenye game ya muziki baada miaka 13 kukosekana kwenye ramani ya muziki.
Bushoke amesema kuwa hawezi kuviweka wazi vitu vingine alivyoongea na mwanamuziki huyo kwani wanasubili mpaka kolabo yao itakapokamilika.
Papii Kocha pamoja na baba yake waliachiwa huru kwa msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli siku ya sikukuu ya Uhuru ambapo kitaifa ilifanyika mkoani Dodoma.