Mbunge wa Bunda mjini, Esther Bulaya amewataka wabunge wenzake kujitoa kwa nafasi walizonazo ili kuwasaidia mabinti wenye uhitaji wa taulo za hedhi (Pedi), kuepuka kukosa kuhudhuria darasani kwa siku zisizopungua 60 kwa mwaka.

Bulaya amesema kwamba kampeni ya Namthamini imemfanya awafikirie mabinti wengi kutoka jimboni kwake na taifa kwa ujumla jinsi wanavyopata wakati mgumu baada ya kushindwa kupata vifaa ya kujisitiri waingiapo kwenye mzunguko wa hedhi.

Mbunge huyo ameahidi ameahidi kuwasilisha ombi lake kwa  serikali katika mkutano ujao wa bunge juu ya kushiriki kikamilifu katika kumtengenezea mwanafunzi wa kike mazingira rafiki ya kuweza kujisitiri pindi wanapokuwa katika hedhi.

Bulaya amekabidhi taulo za hedhi ambazo hakutaja thamani yake akiwa ameongozana na Mbunge wa viti Maalumu Lindi, Lathifa Chande pamoja na pesa taslimu shilingi laki moja kutoka kwa Mbunge wa Kawe, Mh. Halima Mdee na kuahidi kabla ya kufikia tarehe ya kilele  ataongeza vifaa hivyo kwa kadri atakavyojaaliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *