Waziri wa mazingira nchini Burundi, Emmanuel Niyonkuru amefariki baada ya kupigwa risasi mjini Bujumbura saa chache tu baada ya kuingia mwaka mpya.

Police wamesema amepigwa risasi alipokuwa akielekea nyumbani kwake eneo la Rohero nchini humo.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameapa kuchukua hatua kali za kisheria kwa atakayepatikana na hatia ya kuhusika katika mauaji hayo.

Nkurunziza amesema kuwa waliohusika watachukuliwa sheria kali kutokana na tukio hilo la kuuawa kwa waziri huyo.

Mamia ya watu , wakiwemo maafisa wa ngazi za juu katika jeshi wameuawa tangu rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu 2015, hatua ambayo wapinzani wamesema ni kinyume na sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *