Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa ameita kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Ethiopia Oktoba 8 mwaka huu.

Wachezaji hao wataunda kikosi cha stars ambacho kitasafiri mwishoni mwa wiki ijayo kwenda Addis Ababa, Ethiopia kucheza na wenyeji  kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Oktoba 8, mwaka huu.

Mkwasa maarufu kwa jina la Master amesema wachezaji aliowaita wataingia kambini Oktoba 2, 2016 kabla ya kuanza kukiandaa kuanzia Oktoba 3, 2016.

Nyota wa Stars walioitwa na Mkwasa ni Makipa; Deogratius Munishi ‘Dida’ (Yanga SC), Said Kipao (JKT Ruvu) na Aishi Manula (Azam FC).

Mabeki; Shomari Kapombe (Azam FC), Juma Abdul, Andrew Vincent, Mwinyi Hajji (Yanga SC), Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC), David Mwantika (Azam FC) na James Josephat (Prisons).

Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Mohammed ‘Mo’ Ibrahim,
Jonas Mkude, Muzamil Yassin, Jamal Mnyate, Shiza Kichuya (Simba SC), Simon Msuva, Juma Mahadhi (Yanga SC) na Hassan Kabunda (Mwadui FC).

Washambuliaji ni Ibrahim Hajib (Simba SC), John Bocco (Azam FC), Mbwana Samatta KRC Genk (Ubelgiji), Elius Maguli (Oman) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

Mchezo huo ulio katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), utafanyika mjini Addis Ababa, baada ya maombi ya Shirikisho la Soka Ethiopia (EFF).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *