Waziri wa zamani wa Serikali ya Burundi na mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Hafsa Mossi ameuawa kwa kupigwa risasi nchini Burundi.
Mauaji ya mwanasiasa huyo na mtangazaji wa zamani wa idhaa ya Kiswahili ya shirika la utangazaji la Uingereza BBC yametokea kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura muda mfupi uliopita.
Mpaka sasa bado Serikali ya Burundi haijatoa taarifa yoyote kuhusu wahusika wa mauaji hayo ingawa raisi Nkurunzinza ameyaita ‘mauaji ya kupangwa’.
Makundi mbalimbali ya kisiasa na kijamii kutoka nchini Burundi yapo mkoani Arusha (Tanzania) yakiendelea kutafuta suluhu ya machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini kwao.
Burundi imeingia kwenye mgogoro wa kisiasa baada ya raisi Pierre Nkurunzinza kutangaza nia ya kuongeza muhula wa uongozi wake.