Nchi ya Brazil imesherehekea sikukuu kubwa zaidi nchini humo ya ‘Karnivali’ maarufu kama sikukuu ya Matope.

Sikukuu hiyo haijali masikini wala matajiri, nyota wala watu wa kawaida kwani watu wa rika na matabaka tofauti hujimwaga mitaani kusherehekea kwa siku tano.
Mwaka huu ilianza Jumamosi iliyopita, ambapo mitaa ilipambwa na washerehekeaji hao wakiwa na mavazi ya mitindo mbalimbali huku wakicheza na kunywa.
Lakini wakati miji mbalimbali mikubwa ikiwamo Rio de Janeiro hali ikiwa hivyo, mamia ya washerehekeaji walimiminika katika mji wa Paraty wa ufukweni kuogelea matopeni wakati wa maadhimisho hayo.
Kwa mji huo mdogo, kuvaa mavazi ya thamani, manyoya, ngozi na kila aina ya mapambo ambayo huitambulisha Sikukuu ya Karnivali nchini Brazil hayana nafasi.
Watu katika mavazi ya kuogelea topeni katika mji huo, huonekana kama ilivyokuwa Jumamosi iliyopita wakijitupa katika mabwawa ya tope jeusi ndii, lenya utajiri wa madini kwa ajili ya sherehe hizo.
Sherehe hizo za tope zinajulikana kama ‘Bloco da Lama’, maneno ya Kireno yenye maana ya Sherehe za Tope za Mtaani.’

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *