Moja ya mijadala mikubwa ya ubora wa video za wasanii wa Bongo Fleva umekuwanni ubora wa vifaa vya kurekodia pamoja na mandhari husika za kurekodia videobhizo.

Mvutano huo umenasibishwa pia na uwezo wa waongozaji video (Directors) kutoka Tanzania na wale wanaotoka nje ya Tanzania wakiwemo Campos na Godfather. Mashabiki wengi wa muziki kwa ujumla wamekuwa wakivutiwa na kazi ya msanii wampendaye bila kujali sana ilikotengenezwa au aliyeitengeneza ili mradi tu

‘INAWAKOSHA’.

Msuguano huu wa kutengenezwa kwa video zenye ubora pia umekuwaukinasibishwa na maeneo ya kutengenezea video hizo pamoja na fursa za upatikanaji wa ruhusa ya matumizi ya maeneo maalum kwaajili ya kazi hizo.

Hali hiyo imepelekea kwa kiasi kikubwa wasanii wa Bongo Fleva kuanza kukimbilia nchini Afrika Kusini ili kupata vitu vyote hivyo na mwishowe kupata video bora zaidi huku jambo la muhimu zaidi likiwa ni kujitangaza nje ya mipaka ya Tanzania. Swali la kujiuliza ni kuwa, mandhari au amaeneo mazuri ya kutengenezea video hizo kwa hapa Tanzania hayapo?

Je, Serikali kupitia wizara na mamlaka zinazohusika na utangazwaji wa vivutio vya utalii vilivyopo nchini hawaioni fursa hii ya kuwatumia wasanii wa ndani kutangaza vivutio hivyo kupitia nyimbo zao kwa kuwatoza gharama nafuu za matumizi ya maeneo hayo?

Ingawa wasanii wengi wanalalamika kuwa Bongo hakuna maeneo ya kutengenezea video nzuri lakini ukiitazama nyimbo ya Hemedi utakubali kuwa BONGO ina maeneo mengi mazuri.

Video directors kutoka Tanzania jifunzeni zaidi ili UZUSHI huu wa wasanii uondoke!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *