Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kurejesha mfumo wa zamani wakutoa fedha kwa wanafunzi wa chuo.
Waziri Ndalichako amekiri kutokea mapungufu katika mchakato wa ugawaji wa mikopo kwa wanafunzi hao wa elimu ya juu nchini.
Waziri huyo amesema Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu wa Juu imelazimika kubadili mfumo wa utoaji mikopo ili kukabiliana na mapungufu mbalimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na sintofahamu kubwa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika vyuo vikuu nchini baada ya wengi wao kukosa mikopo huku wachache wakipewa kiasi kidogo ambacho kinadaiwa hakitoshelezi.