Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inatarajia kuanza kuwasaka wadai sugu 100,000.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul Badru amesema Januari 8 wataanza kuwasaka wadai hao ambao mikopo yao inafikia Tsh. Bilioni 285.
Amesema kuwa “Kiwango kilichoiva mbacho kipo mikononi mwa hawa sugu ni bilioni 285 na hii inajumuisha wote tangu shughuli za ukopeshaji zilivyoanza, tangu mwaka jana wamefanikiwa kuwapata wadai 26,000 ambao ni sugu,”.
Ameendelea kwa kusema malengo yao ni ifikapo mwezi wa saba mwaka huu makosanyo ya mwezi yaongezeke kutoka wastani wa bilioni 13 hadi 17.