Mwanamuziki ya nyimbo za reggae nchini Uganda, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine amekamatwa na polisi.

Alikuwa akifanya kampeni kama mgombea huru kwa nafasi ya ubunge nje ya mji wa Kampala, kwenye uchaguzi mdogo ambao utafanyika siku ya Alhamis.

Polisi walisema Kyagulanyi alikuwa ameonywa mapema asitumia eneo hilo kwani Rais Yoweri Museven alikuwa karibu na eneo hilo kiasi cha kilomita moja kutoka hapo.

Magazeti ya New Vision na Monitor yanasema kuwa hakukutolewa sababu ya kukamatwa kwake.

Lakini lile la Monitor linasema kuwa wafuasi wake walipambana na wale wa mpinzani wake jana Jumatatu.

Rais Museveni wa chama cha NRM na hasimu wake wa muda mrefu Dr. Kizza Besigye wa FDC, pia na wanatarajiwa kufanya mikutano eneo hilo leo, kuwaunga mkono wagombea wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *