Mkali wa rap Bongo, Mr. Blue A.K.A Kabaiser amekanusha kumdisi mfalme wa Bongo Fleva, Alikiba kwenye wimbo wake mpya ‘Mbwa Koko’.
Blue amefunguka hayo baada ya kuwepo habari katika mitandao ya kijamii kuwa amemdis Alikiba kwenye wimbo wake mpya ambapo amemtaja mkali huyo pamoja na wimbo wake ‘Seduce Me’.
Mr Blue ambaye alitamba na nyimbo kama Mapozi na nyinginezo amedai kuwa sababu kubwa iliyompelekea kumtaja Alikiba katika ngoma hiyo ni kutaka kujiweka mbali na wanawake wanaoshindwa kujistili.
Mbali na Alikiba mwanamuziki huyo pia amewataja wasanii wengine wa Bongo Fleva kama vile, Kassim Mganga, Saida Karoli na wengine wengi.
Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa alichofanya yeye ni majigambo na katika sanaa anayoifanya inamruhusu kufanya hivyo kwa hiyo watu na mashabiki wasichukulie kama ‘diss track’ kwa hao.