Kampuni ya simu ya Blackberry imeishtaki kampuni Nokia kwa madai ya kampuni hiyo kutumia teknolojia ya Blackberry.

Madai hayo ya ukiukaji yanahusisha teknolojia inayotumika katika 4G pamoja na mitandao mingine ya simu.

Kampuni hiyo ya Canada inadai kwamba transmita za Nokia pamoja na programu nyengime zinatumia teknolojia yake.

Blackberry inataka kulipwa fedha badala ya kuizuia Nokia kutumia teknolojia yake kulingana na nakala za mahakamani zilizochapishwa na tovuti ya habari ya Ars Technica.

Madai hayo ni pamoja na yale yanayosema kwamba Nokia ilikuwa inajua uwepo wa uvumbuzi huo baada ya kujaribu kuununua hapo awali kabla ya Blackberry kuamua kutumia.

Kampuni hizo mbili zilizozana 2012 wakati Nokia ilipojaribu kuhakikisha kuwa mauzo ya simu za Blackberry yanapigwa marufuku nchini Marekani na Uingereza katika mzozo mwengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *