Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Billnass amefunguka na kusema kuwa aliyewahi kuwa mpenzi wake Nandy anamchukulia kama dada yake kwakuwa uhusiano wao uliisha kitambo.
Amesema kuwa hawezi kumuita mwanadada huyo ‘Ex’ wake kwakuwa waliachana kitambo na mahusiano yake hayakudumu muda mrefu.
Bilnass amesema kuwa “Nandy ni dada yangu kibusara siwezi kumuita ‘Ex’ wangu kwakuwa nilivyoachana nae nimeingia kwenye mahusiano na wasichana wawili tofauti hivyo historia hiyo imekuwa ya zamani sana”.
Ameendelea kusema kuwa jina hilo ameliona kuwa ndio lenye heshima zaidi kwa wakati huu, msikilize hapo chini Billnas akifunguka Zaidi.