Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Billnass amefunguka na kusema kuwa anashangaa watu wanaosambaza taarifa kwamba ameachana na mpenzi wake Nandy.
Billnass amesema kuwa anashangaa kuona taarifa hizo wakati hajawahi kuongea lolote kuhusu hali yake ya mahusiano kwasasa na mpenzi wake huyo.
Billnass amesema watu wanakosea kusambaza taarifa hizo na wala hazihusiani na kile alichokiimba kwenye wimbo wake mpya wa tatizo ambapo mashabiki wengi wametafsiri kama amemchana Nandy.
“Mimi sijawahi kuzungumza popote kuhusu suala langu la mahusiano na hakuna mtu ambaye nimetaka aone kwamba nieleze ishu ipo hivi au vile, nimeamua kufanya kazi yangu ila tatizo kubwa ni kuanza na ukurasa mpya, watu wanakosea”.
Taarifa za wawili hao kuachana zimeendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii kutokana na wapenzi hao kutoonekana pamoja kwa muda mrefu.