Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Billnass amefunguka na kusema kuwa ana wasiwasi na mashabiki kwamba hawajaelewa kile alichokiimba kwenye wimbo wake mpya wa tatizo ambapo kuna stori inayosemekana amemuimbia Nandy kwa sababu wameachana.
Billnas amesema kuwa “Tatizo ni wimbo unaoelezea ukurasa mwingine mpya na stori halisi pia itakuwa project ambayo inamuendelezo, itachukua muda kuielewa kwa sababu inahusiana na maisha yangu ila nina wasi wasi sana watu hawajaelewa vile ambavyo natamani waelewe”.
Pia amesema kuwa “Ukiisikiliza hii stori na watu ambavyo wanaioanisha ni vitu viwili tofauti, inaweza ikawa inaoana lakini kuna utofauti sana, ni stori endelevu nitaidadavua vizuri kwa sababu ni stori inayoendelea”.
Billnass na Nandy wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu na hadi kufikia hatua ya kuvalishana pete ya uchumba mwaka jana 2020.