Mwanzilishi wa Microsoft, Bill Gates ameongoza orodha ya watu matajiri zaidi duniani mwaka huu.
Kwa mujibu wa jarida Forbes, mali ya za Bill Gates zimeongezeka hadi $86bn, kutoka $75bn mwkaa jana.
Katika orodha hiyo ya Forbes, mabilionea 183 walijipatia utajiri wao kupitia teknolojia, utajiri wao ukiwa jumla ya dola trilioni moja za Marekani.
Wengine walio kwenye 10 matajiri zaidi ni mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos, ambaye amepanda hadi nambari tatu utajiri wake ukiongezeka kwa kiwango cha juu zaidi kuliko wa mtu mwingine yeyote duniani.
Mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg yupo nafasi ya tano na mwanzilishi mwenza wa Oracle Larry Ellison ameeshika.
Idadi ya mabilionea duniani ambao sasa wanafikia 2,043, ilipata ongezeko kubwa zaidi kwa mwaka mmoja katika kipindi cha miaka 31 tangu orodha hiyo ianze kuandaliwa.
Mabilionea kutoka Marekani walikuwa 565, jambo ambalo Forbes wanasema huenda lilitokana na kuimarika kwa soko la hisa pakubwa tangu Trump aliposhinda uchaguzi Novemba 2016.
China ilikuwa ya pili kwa mabilionea ikiwa na mabilionea 319 nayo Ujerumani ya tatu na mabilionea 114.
Watu 10 matajiri zaidi:
- Bill Gates (mwanzilishi mwenza wa Microsoft): $86bn
- Warren Buffett (mwekezaji Mmarekani): $75.6bn
- Jeff Bezos (mwanzilishi wa Amazon): $72.8bn
- Amancio Ortega (mwanzilishi wa Inditex): $71.3bn
- Mark Zuckerberg (mwanzilishi wa Facebook): $56bn
- Carlos Slim (mfanyabiashara kutoka Mexico): $54.5bn
- Larry Ellison (mwanilishi mwenza wa Oracle): $52.2bn
- Charles Koch (mfanyabiashara Mmarekani): $48.3bn
- David Koch (mfanyabiashara Mmarekani): $48.3bn
- Michael Bloomberg (mwanzilishi wa Bloomberg): $47.5bn