Imebainika kuwa wamiliki wa klabu ya Liverpool ya Uingereza na uongozi wa timu hiyo ulijaribu kuwasiliana na tajiri wa Marekani, Bill Gates ili kumuuzia timu hiyo.

Maelezo hayo yamekuja kuwekwa wazi kwenye nyaraka zilizowasilishwa mahakamani kuhusiana na mgogoro wa kisheria unaendelea baina ya Mill Financia, mmiliki mwenza wa zamani, George Gillet na Royal Bank of Scotland.

Hata hivyo nyaraka hizo zinaonyesha kuwa Gates anayekadiriwa kuwa na utajiri unaofikia £70bn (TZS195tn) hakujibu maombi aliyotumiwa.

Mbali ya Gates, pia maombi mawili ya kuinunua Liverpool yalitumwa kwa mmiliki wa timu ya mchezo wa mpira wa miguu wa Marekani, New England Patriots ambaye hata hivyo alikataa haraka kuinunua timu hiyo.

Imetajwa mahakamani hapo kuwa Gillet na mmiliki mwenza, Tom Hicks walioinunua timu hiyo ya Anfield mwaka 2007, lakin wakakubaliana kuiuza mwaka 2010 waliiteua kampuni ya Barclays Capital kuwatafutia wanunuzi wa klabu hiyo.

Sir Martin Broughton aliyekuwa mwenyekiti wa lIVERPOOL WAKATI HUO alipoulizwa endapo kulifanyika jitihada ya kutafuta wanunuzi Marekani ikiwemo kuwasiliana na Bill Gates na Bob Kraft, alijibu ‘sahihi’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *