Mzee mweye umri wa miaka 91 kutoka nchini Thailand amepata shahada yake baada ya masomo yaliyomchukua karibu miaka 10.

Kimlan Jinakul amekuwa na ndoto wa kujiunga na chuo kikuu tangu awe mtoto lakini hakupata fursa hiyo.

Lakini miaka mingi baadaye baada ya kuwasomesha watoto wake hadi vyuo vikuu, aliamua kujiunga na chuo na siku ya Jumatano amefanikiwa kupata shahada yake.

Kimlan ambaye anatokea mkoa wa Lampang kaskazini mwa Thailand. Alikuwa mwanafunzi mwenye kuelewa masomo na alisomea kati ya shule bora zaidi mkoani humo.

Lakini hakufanikiwa kuendelea hadi chuo kikuu wakati huo na baada ya familia yake kuhamia mji wa Bangkok, aliolewa na kaachana na ndoto yake ya kusoma zaidi.

Watoto wake wanane kati ya watano wana shahada za uzamili na mmoja amefanikwa kupata shahada ya uzamifu au PhD nchini Marekani.

Wakati mmoja wa mabinti zakae ambao walikuwa wakifanya kazi hospitalini walianza kusoma katika chuo cha Sukhothai Thammathirat nao waliamua kujiunga.

Alikuwa na umri wa miaka 72 wakati alijiunga na chuo kiuu, lakini kufuatia kifo cha moja wa mabinti zake aliacha masomo kwa miaka kadha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *