Raia wa Afrika wanaojaribu kuvuka na kuelekea barani Ulaya, wanauzwa na watekaji wao na kuuzwa katika soko la utumwa nchini Libya.

Hayo yamesemwa na shirika la kuwahudumia wahamiaji duniani International Organization for Migration (IOM).

Wahathiriwa wameiambia IOM kuwa, baada ya kuzuiliwa na walanguzi wa biashara ya watu au makundi ya wapiganaji, wanapelekwa hadi kwenye viwanja vya mji au kwenye maeneo ya kuegeshea magari na kuuzwa.

Kiongozi mkuu wa shirika hilo la IOM nchini Libya, amesema kuwa wahamiaji walio na ujuzi kama vile upakaji rangi au ukulima, wanauzwa kwa bei ya juu.

Libya imekuwa katika ghasia tangu mwaka 2011 pale wanajeshi wa shirika la kujihami la mataifa ya magharibi-NATO yalipomuondoa madarakani Rais wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi.

Kwa mjibu wa IOM, maelfu ya wanaume  kutoka mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara wameuzwa katika masoko hayo ya utumwa wa binadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *