Rais wa Benki  ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim amesema kuwa Benki ya Dunia inatarajia kutoa kiasi cha Shilingi Trilioni 1.7 kwa Tanzania kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ya huduma za jamii ikiwemo elimu.

Hayo amesema jana Jijini Dar es Salaam alipotembelea Shule ya Msingi ya Zanaki ya Jijini Dar es Salaam, ambayo ni moja kati ya shule zinazonufaika na fedha za Benki ya Dunia.

Amesema msaada huo ni mkopo wenye lengo la kuisaidia Tanzania katika uboreshaji wa miundominu ya elimu hasa maeneo ya vijiji yasiyofikiwa kwa urahisi na huduma hiyo kutokana na miundombinu mibovu.

Dkt. Kim amesema Benki ya Dunia itaendelea kuisaidia Tanzania kwakuwa ni moja ya nchi inayotumia vizuri fedha inazozitoa na kujiletea maendeleo kwa wakati na kuzitaka nchi nyingine zijifunze matumizi mazuri ya fedha za misaada kutoka kwa Watanzania.

Akizungumza wakati wa makubaliano hayo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philipo Mpango amesema serikali itahakikisha fedha hizo zinaenda kuboresha miundombinu ya elimu ili kuhakikisha taifa linapiga hatua katika sekta ya elimu na kufikia malengo ya milenia katika sekta hiyo waliojiwekea.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema wana mpango wa kuendelea kujenga zaidi shule kwa kuwa elimu ya bure imeongeza idadi ya wanafunzi hivyo bado kuna changamoto ya vyumba vya madarasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *