Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amefunguka na kudai kuwa hakuna faida yeyote aliyoipata baada ya kutoa albam kwani mashabiki hawatoi sapoti.
Ben Pol amewataka mashabiki kuwa wazalendo katika kutoa ushirikiano kwa wasanii wanao wapenda ili mradi waweze kufika sehemu wanayostahiki.
Kauli hiyo ya Ben Pol imekuja baada ya kuwepo upepo wa wasanii wengi kukimbilia kutoa albamu za muziki bila ya kufanya tathimini ya soka lilivyo kwa nyakati hizo.
Ben Pol amesema kuwa kwasasa bado ni changamoto katika soko la filamu kwasababu mashabiki hawatoi sapoti katika ununuzi wa albam.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa hapo hawali tatizo lilikuwa kwa wasanii kutotoa albam lakini kwasasa tatizo ni kwa mashabiki wanashindwa kununua albam hizo za wasanii nchini.