Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben pol amefunguka na kusema kuwa kwa muda sasa amekuwa akihudhuria harusi za wasanii wenzake na yeye anapata moyo wa kutamani kufunga ndoa kama wenzake na anaamini kuwa Mungu ni mwema na yeye atakamilisha ndoa yake hivi karibuni.
Ben Pol ameongea hayo siku ya harusi ya msanii mwenzao stamina ambapo wasanii kadhaa walikuwemo akiwemo Young Killer pamoja na Roma.
Ben Pol nasema kuwa amekuwa akipata moyo wa kuoa mara kwa mara na anaona kabia zamu yake imefika ili pia watu waweze kuja kwake na kusherekea kama vile ambavyo yeye amekuwa akienda kufanya hivyo kwa wenzake na anaamini kuwa yatatimia .
Stamina na mpenzi wake wa siku nyingi walifunga ndoa wikiendi hii na ndoa hiyo kusimamamiwa na msanii Roma ana mke wake huko mkoani Morogoro.