Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amefungua shauri la talaka Mahakamani dhidi ya Mke wake Anerlisa kutokea Kenya, shauri hilo limefunguliwa katika Mahakama moja ya Mwanzo Jijini Dar es Salaam.
Ben na Anerlisa kati ya couple maarufu Afrika Mashariki, baada ya uchumba wao kwa muda walifunga ndoa mwezi Mei mwaka jana katika Kanisa Katoliki la St. Gaspar Mbezi Beach, Dar es Salaam.
Hatau hii ya Ben Pol kugunfua shauri la talaka linakuja siku chache baada ya mrembo Anerlisa kuondoa utambulisho wa maelezo kwenye Ukurasa wake wa Instagram wa kuwa wawili hao ni mke na mume.
Shauri hilo limefunguliwa na Benard Paul Mnyang’anga katika Mahakama moja ya Mwanzo Jijini Dar es salaam, hata hivyo bado haijafahamika sababu za Mwimbaji huyu kuamua kuivunja ndoa hiyo.
Ben Pol na Anerlisa walifunga ndoa mwishoni mwa mwezi May mwaka 2020 katika Kanisa Katoliki la St. Gaspar Mbezi Beach, Dar es salaam na kuhudhuriwa na Watu wachache kutoka upande wa familia zote mbili pamoja na Marafiki wachache wa karibu wa familia.