Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Beka Flavour amefunguka juu ya tetesi zinazosambaa kuwa amemwagana tena na mkewe anayejulikana kwa jina la Happyness.
Beka Flavour anasema kuwa, katika maisha yake hajawahi kuoa na anachokijua yeye Happy ni mzazi mwenzake na wala siyo mke wake, hivyo haoni sababu ya kumuongelea, lakini ambacho watu wanatakiwa wakifahamu kwa sasa kuhusu yeye ni kwamba yupo singo.
“Mimi sijawahi kuoa na wala sina mpango wa kuoa leo wala kesho hivyo watu wasikae na kusema hivyo kwa kuwa sijawahi kuoa, alisema msanii huyo.
Kwa hiyo sina mke ila ninachokijua ni kwamba nina mwenzangu ambaye kwa sasa tumebaki kulea tu mtoto wetu, hivyo jimbo liko wazi, kwa ufupi nipo singo,” anasema Beka anakimbiza Ngoma ya Bahati Mbaya.