Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Beka Flavour amefunguka na kusema kuwa hajatetemesha na ujio wa mwanamuziki Maromboso kutoka WCB ambaye walikuwa wote Yamoto Band.

Kauli hiyo ya mwanamuziki huyo inakuja kufuatia baadhi ya mashabiki wa mziki nchini kudai Beka anahofia ujio wa Maromboso ambaye kwasasa yupo chini ya WCB inayoongozwa na Diamond Platnumz.

Pia Beka amesema kuwa yeye kama msanii hawezi kumuogopa mwanamuziki mwenzake yoyote kwasababu anajiamini.

Kwa upande mwingine Beka fleva ameongelea tetesi za yeye kukasirikia mafanikio ya Mbosso kusainiwa WCB na hivyo kusababisha kutohudhuria halfa yake ambapo amedai alichelewa kupata taarifa za shughuli hiyo hali iliyopelekea kushindwa kufika.

Beka flavour, Aslay, Mbosso na Bella waliunda kundi la Yamoto band waliojipatia umaarufu miaka ya nyuma kabla ya kila mmoja kufanya kazi kivyake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *