Bei ya nyanya katika masoko mbalimbali Jijini Dar es Salaam imepanda kulinganishwa na hali ilivyokuwa wiki mbili zilizopita.

Kwasasa bei ya jumla imepanda kutoka shilingi elfu 35 kwa sanduku na kufikia shilingi elfu 60 tofauti na hali ilivyokuwa nyuma.

Baadhi ya madalali wamesema kuwa bei imepanda kutokana na kiasi kidogo cha shehena ya nyanya kinachoingia sokoni hapo kwa sasa wanategemea nyanya kutoka kwa wakulima wa Arusha, Iringa na Makambako pekee.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wadogo wanaouza nyanya kupitia vipimo vya asili maarufu kama sado, wamesema kupanda kwa bei kumefanya biashara kuwa ngumu kwani wateja wamekuwa hawamudu ongezeko hilo la bei.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *