Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limesema kitendo cha mwanamuziki Diamond Platnumz kuimba wimbo wa Mwanza uliofungiwa na baraza hilo ni dharau na kubainisha kuwa litatoa tamko kuhusu kitendo hicho.
Diamond aliimba wimbo huo alioshirikishwa na Rayvanny jana Desemba 15, 2018 katika tamasha la Wasafi lililofanyika jijini Mwanza jana, huku maelfu ya mashabiki wakimshangilia na kumfuatisha alivyokuwa akiimba.
Mwanamuziki huyo aliimba wimbo huo jukwaani akiwa pamoja na Rayvanny mwanamuziki wake Rayvanny.
Katibu mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza amesema, “Nimepigiwa simu kuhusu hii kitu. Niko Arusha kikazi nimeshawasiliana na mwenyekiti wa bodi ya Basata.”
Wimbo huo ulifungiwa Novemba 12, 2018 na baraza hilo kwa maelezo kuwa unahamasisha masuala yasiyokubalika katika jamii.