Barua za mapenzi ambazo ziliandikwa na Barrack Obama kwa mpenzi wake alipokuwa kijana zilidhihirisha wasiwasi wake kuhusu ubaguzi wa rangi, tabaka na fedha.

Barua hizo zilizoandikwa kwa mkono zilikuwa kati ya Obama alipokuwa mdogo na mpenziwe wakati huo Alexandra McNear ambaye alikutana naye katika jimbo la California.

Baadhi ya barua hizo zinaonyesha hali ngumu ya maisha na kazi aliyofanya ambayo hakuipenda.

Barua hizo zilizochukuliwa na maabara ya chuo kikuu cha Emory University mwaka 2014 na sasa ni mara ya kwanza kuchapishwa.

Ziliandikwa vizuri na zinafichua utambulishi wa kijana huyo , mkurugenzi wa maabara hiyo Rosemary Magee alisema.

Zinaonyesha maswala ambayo wanafunzi wanakabiliana nayo na kwamba wanafunzi wote hupatikana na matatizo kama hiyo.

Uhusiano wa kuishi mbalimbali:

barua hizo ziliandikwa kati ya 1982 na 1984 miaka mitano kabla ya Obama kukutana na mkewe Michelle Obama.

Katika mojawapo ya barua hizo aliandika: Naamini unajua kwamba natamani kukuona na kwamba wasiwasi wangu kwako ni mkubwa kama vile hewa, Matumaini yangu kwako ni sawa na kina cha bahari, penzi langu ni kubwa kwako.

Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Barrack Obama

Ilitiwa saini: Mpenzi Barack.lakini uhusiano wa mbalimbali hakuendelea.

Kufikia 1983, alimwambia: Nakufikiria kila mara ijapokuwa nakanganyika kuhusu hisia zangu.

Inaonekana tutataka kuwa na kile ambacho hatutakipata , na hicho ndio kinachotuunganisha na ndicho kinachotutenganisha.

Katika barua moja, Obama aliandika kuhusu marafikize waliokuwa wanajiandaa kuanza maisha ama kusimamia biashara za familia zao.

Lakini akiwa mzaliwa wa Hawaii, na baba kutoka Kenya , kutumia muda wake mwingi wa ujana wake nchini Indonesia alihisi tofauti.

Nikiwa bila tabaka, nguzo, ama hata utamaduni , hatua ya kuchukua mwelekeo tofauti ipo mbele yangu.

Njia pekee ya kuchochea hisia zangu dhidi ya upweke huu ni kukumbatia utamaduni, tabaka.lakini haikuwa rahisi.

Baada ya kuhitimu 1983, kurudi India nilikokulia , aligundua kwamba hatoki katika eneo hilo.

Siwezi kuzungumza lugha hiyo kwa ufasaha wowote.

Watu hawanieleiwi , kutokana na tofoauti yangu na wananidharua kwa sababu mimi ni M’marekani.

Nakumbana na barabara mbovu, nyumba za mabanda ,barabara zangu za zamani siwezi kupitia.

Kijana huyo anajua kwamba alitaka kufanya kazi katika miradi ya jamii ambayo baadaye angepigania akiwa rais, lakini kama vijana wengine wengi alilazimika kufanya kwa vitendo.

Wiki moja siwezi kulipia ada ya kutuma barua, mara nyengine nakosa hundi ya kununua tapureta, aliandika 1983.

Mshahara katika mashirka ya kijamii ni ya viwango vya chini mno kuweza kuendelea kutegemea kwa hivyo nalazimika kufanya kazi za ziada kwa mwaka ili kuweza kuhifadhi fedha ili kupigania maslahi yangu.

Nilipopata kazi katika kampuni ya uchapishaji , anasema alikuwa mmoajawapo ya vijana waliosifiwa kwa kazi nzuri huku kila mtu akinipongeza kwa kazi yangu nzuri.

Na pia kuna ishara nyengine katika maandishi yake kuhusu vile angetaka kuwa siku za usoni.

Mwaka 1984 katika barua kwa Alexandra alifikiria kuhusu vile ambavyo angeutumia ushawishi wake katika siku za usoni.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *