Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barnaba amesema kuwa mwakani anatarajia kusaini wasanii wa kike watatu kwenye lebo yake ili kuinua muziki kwa upande wa wanawake.

Banarba amesema kuwa anahitaji wasanii wa kike watatu kwani wa kiume tayari wapo wengi katika industry ya muziki Bongo hivyo anahitaji kuinua vipaji kwa upande wa wasanii wa kike nchini.

Mwanamuziki huyo ambaye ni zao la THT amesema kuwa kwasasa lebo yake bado changa kwa hiyo ataanza kwa wasanii wa tatu na hapo baadae atachukua wasanii wengine kwenye lebo yake hiyo.

Barnaba amesema kuwa kwasasa lebo hiyo ina mwanamuziki wa kiume mmoja anayefahamika kwa jina la Mula alisainiwa mapema mwaka huu.

Pia Barnaba amesema kuwa msanii wa kiume atabaki Mula peke yake kwasababu wanaume wapo wengi kwenye game la muziki nchini tofauti na wanawake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *