Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barnaba amewataka baadhi ya wasanii kuacha tabia ya kutumia kiki katika muziki wao kwani kufanya hivyo ni kujishusha kimuziki.

Kauli ya mwanamuziki huyo imekuja kufuatia baadhi ya wasanii kutumia kiki ili kukuza kimuziki wao jambo ambalo uwaondolea sifa katika jamii kutokana na vitendo vya kutafuta kiki ili kujulikana zaidi kwa mashabiki wao.

Barnaba amesema kuwa “Baadhi ya wasanii wanapenda kufanya kiki na kwa upande wangu naona ni utoto maana msanii ni kioo cha jamii na wengi wanaokutazama ni watu walionyuma yako na wanakutazama kama mfano wao wa kuiga hivyo kama ukizoea kufanya ‘kiki’ basi watu watakuchukulia hivyo.

Pia amesema kuwa “Mimi ni muoga kufanya kiki na nimelelewa kwenye familia ya maadili kuanzia nyumbani mpaka kwenye muziki wangu na kuna watu wengi wananipenda hivyo siwezi kuibomoa thamani yao kwangu kwa story za muda mfupi”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *