Staa wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema kabisa na albamu yake ya ‘Gold’ amewajia juu watu ambao wamekuwa wakitumia vibaya mitandao ya kijamii.

Serikali imekuwa ikikemea vikali matumizi mabovu ya mitandao ya kijamii kwani Kumekuwa na watu wanaofanya uharibifu na mitandao hiyo ikiwemo kutoa kugha chafu za matusi na hata kuikashifu Serikali.

Mwezi uliopita Serikali Kupitia TCRA walitangaza kuwateua wasanii kama Barnaba, Hamisa Mobetto na wengineo kuwa mabalozi wa kuhakikisha kunakuwa na matumizi bora ya mitandao ya kijamii.

Barnaba Boy Classic ametoa Kauli yake  kuhusu harakati zake lakini kubwa zaidi ni kauli yake kwa watanzania ambao wanatumia vibaya mitandao ya kijamii na yeye  akiwa kama balozi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA ).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *