Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barnaba Boy amempongeza aliyekuwa mpenzi wake Zuwena kwenye siku yake ya kuzaliwa licha ya kuachana naye.

Barnaba na mwanamke huyo walikuwa na uhusiano kwa muda mrefu na hata kubarikiwa kuzaa mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Steven.

Barnaba kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika maeneno ya kuvutia kwa ajili ya mzazi mwenzake huyo.

Wewe ni rafiki yangu na ndugu yangu na uvungu wa moyo wangu nakushukuru kwa kuwa daraja kwenye maisha yangu nashukuru nimevuka Salama, matatizo ni sehemu ya kila mwanadamu, upendo wangu juu ya zawadi uliyonipatia iko pale pale (Steve) na kitu kizuri ninakuheshimu sana mbali na mambo yote na kitu kingine furaha yangu kukuona kutabasamu hata kama hilo tabasamu silitengenezi mimi lakini angali unatabasamu basi nafurahi kukuona, nakutakia maisha mema yenye baraka nawaombea heri katika familia yako nakuombea heri na uwahi uwe shuhuda wangu nami niwe shuhuda wako Wa kila jambo heri. Heri ya kuzaliwa Mama Steve, mama watoto , mzazi mwenzangu damu ya Yesu ikuangaze milele”.

Barnaba na Zuu waliachana baada ya kuwa wrote kwa miaka mingi, baada ya kuweka ujumbe huu mashabiki wengi walijitokeza na kumshauri Barnaba arudiane na Zuu ili walee mtoto wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *