Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barnaba ametoa taarifa rasmi kuwa yuko katika maandalizi ya album yake mpya anayotarajia kuiachia siku za usoni na kwamba mpaka sasa imefikia kwenye hatua nzuri.

Barnaba amedai kuwa anachokiandaa kwenye album hiyo kitakwenda kuandika historia ya kipekee kutokana na namna alivyoamua kuifanya ya tofauti kwa kuwa ndio album yake pekee aliyochanganya mawazo yake na ya watu wengine.

Wasanii wengi aliowashirikisha ni wapya kwenye kiwanda cha muziki wa bongo fleva katika kuikamilisha album hiyo ambayo bado hajaweka wazi tarehe rasmi atakayoiingiza sokoni.

“Album yangu itakuwa bora kwa mwaka 2022 kwa sababu tatu, kwanza ni muziki uliotimia, second nimetoa nafasi kwa new generation kunipa mchango wa mawazo.

Lakini pia ndio album yangu ya kwanza kupata nafasi ya kushirikisha wenzangu wengi kutoka ndani na nje ya nchi pia, i can’t wait wallahi bado naendelea kurekodi na nafanya final when i’m ready nitarudi kuwapa muongozo.”

Barnaba ameyasema hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa mtandao wa Instagram (Insta story) kuhusu taarifa ya albam hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *