Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah amedai hana tatizo na Gigy Money kwa kuwa yeye amechangia kumuweka hapo alipo hivi sasa.
Barakah amesema kuwan yeye ndiye aliyekuwa mtu wa mwanzo kabisa kumuweka kwenye video yake inayoitwa Siachani Nawe.
“Nilimfahamu Gigy Money kama chawa wa Video Vixen wa video yangu ya Siachani Nawe iliyotoka Juni 18, 2015, lakini cha zaidi kabisa ni kwamba Gigy ni mdogo wangu hivyo siwezi bishana na mtoto wa kike,” amesema Barakah.
Msanii huyo ameanika pia sababu za EP yake iliyokuwa ikitarajiwa itoke mwezi Machi, mwaka huu lakini ikashindikana.
“Nimeshafanya EP, hivyo nimeona raundi hii nije kitofauti na si kufanya kama nilivyowahi kufanya huko mwanzo, mwezi huu mashabiki wangu wategemee makubwa maana naachia package yangu ya hatari,” amesema Barakah.