Msanii wa Bongo Fleva, Baraka The Prince  amesadikika kusajiliwa na lebel kubwa nchini ya  Wasafi (WCB) baada ya kuachana na lebo ya RockStar4000.

Wakithibitisha taarifa hizi  katika ukurasa wao wa instagram ,  lebel ya Wasafi waliweka picha ya msanii huyo  Baraka the Prince na kuandika “welcome to the family @barakatheprince -can you tag his fans please” k ikiwa kama njia ya kuthibitisha na  kuwaambia mashabiki kuwa Baraka the Prince yuko Wasafi kwa sasa.

Kwa kipindi cha nyuma kidogo Baraka the Prince alikuwa akionekana kuwa karibu na Alikiba na kusemekana  kuwa wote  wawili walikuwa wasanii  wanaofanya kazi chini ya menejimenti moja yenye jina kubwa duniani inayojulikana kama lebel  ya  Rock Star4000, lakini baadae haikujulikana kimetokea nini lakini tetesi zilisema kuwa Baraka the Prince ameshatoka katika  lebel iyohuku sababu ya kutoka katika lebel iyo ikiwa haijajulikana.

Baada ya tetesi za kutoka katika lebel hiyo kusambaa, kulikuwa na sintofahamu ya maelewano kati ya alikiba na baraka ambao walikuwa wakifanya kazi chini ya menejiment moja , bifu ambalo pia ommy dimpozi alihusishwa kwa sababu kipindi hicho ommy dimpozi pia alikuwa amesajiliwa katika lebel hiyo, ilhali wao wenyewe hakuna hata mmoja aliyetaka kuthibitisha tetesi hizo zaidi ya kukataa na kusema kuwa wao hawana ugomvi wowote.

Ujio wa nyimbo mpya ya Baraka the Prince pamoja na kuhamia wcb inathibitisha kuwa kweli Baraka hayupo tena katika lebel moja na Alikiba lakini je, swali la kujiuliza ni kwamba Wcb ni lebel iliyopo chini ya Diamond Platinumz ilihali Baraka alikuwa akifanya kazi katika lebel moja na Alikiba, je hakuna lolote linalohusisha ugomvi wa team hizo mbili uliopelekea msanii huyo kuhamia huko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *