Mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu, Harmonize aliweka bango lake na Kajala maeneo ya Kinondoni-Manyanya jijini Dar.

Harmonize amesema bango hilo lenye maandishi ya Lovers lilimgharimu shilingi milioni 12  za Kitanzania.

“Niliweka mimi 100%. Nilitumia milioni 12. Itakuwa pale kwa takriban miezi sita,” alisema Harmonize.

Mapema mwezi Aprili, 2022, Harmonize alikwenda kwenye duka la vito na kununua mkufu wa thamani ambao Kajala alikuwa ameupenda enzi za uhai wa penzi lao.

Harmonize alisema alitumia shilingi milioni tano za Kitanzania kupata cheni hiyo.

“Ni tamu sana kutumia pesa zako kwa mtu unayependa.

Hata baada ya hayo yote, Kajala hakusema hata neno moja kuhusu mambo ya Harmonize.

Jana Jumapili Aprili 17, 2022, Kajala alitoa ujumbe ambao baadhi ya walimwengu wamedai kwamba alikuwa anamjibu Harmonize.

Kajala anasema kuwa heri mtu kuishi peke yake kuliko kuwa na mtu mbaya au asiyemfaa.

“Mfano mwema wa heri kuwa peke yako kuliko kuwa na mtu mbaya au asiyekufaa,” anasema Kajala akiambatanisha ya matunda mawili ambapo moja limeharibika na limeanza kuharibu lingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *