Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baby Madaha amefunguka na kukanusha taarifa za kutimuliwa kwenye nyumba aliyopanga baada ya kushindwa kulipia kodi nyumba hiyo.

Baby Madaha amekanusha taarifa hizo zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa ameshindwa kulipa kodi mpaka kupelekea kufukuzwa na mwenye nyumba na kuamua kuamua kuhamia kwa rafiki yake Isabela Malisa.

Taarifa za msanii huyo kufukuzwa kwenye nyumba aliyopanga zilisambaa katika mitandao ya kijamii mpaka kupelekea mashabiki zake kudai kushtushwa na taarifa hizo za mwanamuziki huyo.

Baby Madaha amesema kuwa habari hizo hazina ukweli wowote kwani zinasambazwa na watu wasiomtakia mema na wenye chuki na yeye kwa nia ya kumuharibia katika jamii.

Mwanamuziki huyo kwasasaa ana muda mrefu ajatoa wimbo mpya kwa zaidi ya miaka miwili mpaka kupelekea kufulia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *