Meneja wa Wasafi (WCB) Babu Tale ameweka wazi kuwa msanii Rayvanny bado yupo chini ya lebo hiyo kwa sababu bado hajakamilisha utaratibu wa kujiondoa.
Babu Tale ametoa kauli hiyo ikiwa ni miezi kadhaa baada msanii huyo kutangaza kuwa amejiondoa rasmi WCB.
“Rayvanny amekua amekuja Wasafi akiwa hana uwezo akafanya biashara na Wasafi na sasa hivi ana majumba na anajiweza na amefungua record label yake, leo hii Rayvanny anataka kwenda kuendelea na biashara yake mwenyewe.
“Biashara iko wazi na ruhusa ya kununua haki/hisa zake kwetu ndio hicho tunachokisubiria kikamilike, yupo kwenye mchakato ila tumempa uhuru wa kufanya kazi zake mwenyewe.
“Kama hivi mnaona tumemruhusu anafanya show mwenyewe kila kitu mwenyewe kwa hiyo tunasubiria kila kitu kikamilike anakwenda kujitegemea kwahiyo ni vitu ambavyo vipo kwenye utaratibu.
“Vanny wakati anaenda Wasafi hajaenda kusaidiwa ameenda kufanya biashara na biashara yake imekuwa anakwenda kuwasaidia kina #Macvoice (bado hajamalizana na Wasafi) ni utaratibu tu ujue kumalizana sio kama taa paap kwasababu bado kila kitu kipo chini ya wasafi mpaka leo,” amesema Babutale.