Meneja wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Babu Tale amemshauri mwanamuziki Ruby kutambua tatizo lake ili kurudisha heshima yake.

Kauli hiyo ya Babu Tale imekuja kufuatia ukimya wa mwanamuziki huyo baada ya ya kutotoa kutoa ngoma yoyote zaidi ya kuonekana kwenye mitandao ya kijamii.

Mziki wa Ruby ulianza kulega lega pale alipoamua kujitoa kwenye jumba la vipaji Tanzania (THT) ambapo sanaa yake mwanzoni kabisa aliianzia kwenye jumba hilo lakini mwishoni alipishana kidogo na mabosi zake huko THT  na kuamua kujiengua.

Ruby alionekana akiimba wimbo wa dini kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo wasanii mbali mbali walikiri kuikubali sauti yake na kukikubali kipaji chake wakiwemo Kajala, Jacqueline Wolper, Shetta pamoja na Babu Tale.

Babu Tale kupitia ukurasa wake wa Instagram aliiposti video hiyo na kuisindikiza na ujumbe uliomtaka Ruby kujua anasumbuliwa na ugonjwa gani kulitatua na kisha atapata heshima yake kwenye muziki anaofanya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *