Meneja wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kusema kuwa Rayvanny na mpenzi wake Fayma hawakuachana bali wawili hao walipishana kauli.

Kuali hiyo ya Babu inakuja kufuatia taarifa za kuachana kwa wapenzi hao ambao wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume.

Babu Tale amesema kuwa wawili hao wapo pamoja kama kawaida ila wapishana kauli kama walivyo watu wengine kwani ni jambo la kawaida kwa wapenzi kugombana na kupatana ila hawakuachana na taarifa zinavyoenezwa.

Taarifa za kuachana zilizagaa katika mitandao ya kijamii baada ya wawili hao kurushiana maneno na kupelekea watu kudhani kuwa labda wawili hao wameachana.

Rayvanny ndiyo wa kwanza kurusha picha za wasichana wengine lakini kilicho washangaza watu wengi ni kitendo cha wawili hao kugombana na kuamua kuachana kwenye Instagram.

Babu Tale ambaye ni Meneja wao alifunguka na kudai sio kweli kuwa wawili hao wameachana ila tu kilichotokea ni walipishana kauli na kutoelewana kidogo ila wapo sawa kabisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *