Mwanamuziki wa dansi, Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanaye Jonhson Nguza ‘Papii Kocha’ leo wamekutana na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana Shonza pamoja na wanahabari.

Akizungumza na wanahabari katika Studio za Wanene Entertainment zilizopo Mwenge, Naibu Waziri Shonza amesema wao kama wizara kazi yao kubwa ni kuwasaidia wasanii na kuhakikisha wanafanikiwa kufikia malengo yao, hivyo wameamua kuwakutanisha na wadau wa muziki wakiwemo Wanene ili kufanmikisha zoezi la nguli hao kurudi kwenye game.

Naibu waziri amesema kuwa “Sisi kama wizara kuna namna ambayo tunaitumia kuwasapoti wasanii, hatuwezi kutoa fedha, hivyo tumeamua kuwakutanisha Babu Seya, Papii Kocha na Studio ya Wanene ili waweze kuweka mipango sawa kwa ajiri ya kuendeleza muziki,”.

Kwa upande wake Babu Seya alisema mashabiki wao watulie kwani mipango ndo inapikwa hivyo mambo yakikamilika kila kitu watakiweka hadharani.

Nae mmiliki wa Studio za Wanene, Dash alisema wao wamejipanga kutoa sapoti ya ainza zote kwa babu Seya na papii ili kuhakikisha wanarekodi kazi nzuri na kuzifikisha kwa jamii na mashabiki wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *