Mwanamuziki mkongwe wa dansi nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ amesema kuwa kwa upande wake hana mpango wa kufanya show Zaidi.
Babu Seya amesema kuwa kwasasa show nyingi zitafanywa na mtoto wake Papii Kocha na yeye atakuwa akifanya shughuli za studi zaidi.
Babu Seya aliyekaa jela miaka 14 amesema kuwa kwasasa atafanya show kwa ajili ya kuwashukuru watanzania waliomuombea wakati alipokuwa akitumikia kifungo cha maisha jela katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Kwa upande mwingine Babu Seya amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika ukumbi wa Kings Solomon kwa ajili ya kushuhudia show yao kwa mara ya kwanza toka watoke jela.
Babu Seya na mwanae Papii Kocha walihukumiwa maisha jela mpaka walipotoka kwa msamaa wa Rais Magufuli mwaka jana kwenye sherehe ya sikukuu ya Uhuru.