Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baba Levo amefunguka na kusema kuwa anamshauri Kajala asirudiane na mpenzi wake wa zamani, Harmonize.

Kauli hiyo ya Baba Levo imekuja baada ya kuenea habari mitandaoni kuwa Harmonize anataka kurudiana na Kajala ambaye waliachana mwisho mwa mwaka jana.

Baada ya Harmonize kuandika kwenye Insta Stories zake akimtaka Kajala kumsamehe na kumrudia ili waendelee kulisukuma gurudumu la mapenzi, baadaye Baba Levo amejitokeza wazi na kumtaka Kajala asikubali hata kidogo.

Baba Levo ameposti picha Kajala kwenye Instagram yake na kuandika; “Usikubali!”

Harmonize kipindi kile akiwa katika uhusiano na Kajala alijaribu tena kumvizia mwanawe Paula ambaye wakati huo bado ni mpenzi wa msanii Rayvanny, Baba Levo alimchamba Harmonize kwa maneno makali mpaka kuachia ngoma ya kumtukana Harmonize.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *