Muigizaji wa Bongo Movie, Haji Adam maarufu kama Baba Haji amefunguka na kusema kuwa aliwahi kuwa na mahusiano na muigizaji mwenzake, Aunty Ezekiel kipindi cha nyuma.

Baba haji amesema kuwa yeye na Aunty Ezekiel walikuwa  na mahusiano ya mapenzi kwa muda mrefu na walikuwa karibu sana.

Baba Haji ameongeza kwa kusema kuwa hata kama wamegombana lakini hawawezi kuacha kuongea na Aunty Ezekiel kwa sababau wanaheshimiana sana.

Hata hivyo katika maongezi yake alisema kuwa anatambua wanaume wengi wamepita na mwanadada huyo lakini katika hao ni yeye tu ndo aliyekuwa akimjua vizuri , hata hivyo ameongezea na kusema kuwa anajua kuwa Aunty pia alishawahi kutoka na Kanumba.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wameonekana kukwazika na kitendo hicho cha msanii huyo kuongelea mahusiano yake na msanii huyo ambae sasa hivi anafamilia yake na mume wake pia, hata hivyo wengine waliendelea kuchukizwa na tabia ya Haji Adam kuanza kutaja wanaume aliotembea na dada huyo maana hayo ni maisha yake binafsi.

Aunty Ezekiel kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja na amekuwa na mahusiano ya muda mrefu na baba mzazi wamtoto wake huyo anaejulikana kama Moze Iyobo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *