Baada ya kupata dili la ubalozi wa Kombe la Dunia na Star Times, siku ya jana Wema Sepetu alamba dili linguine na Tatu Mzuka.
Kampuni ya The Network ambayo inahusika na kuendesha Michezo ya namba ya Tatu mzuka, imetangaza kuingia kwenye ushirikiano wa kibiashara na Wema.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Tatu Mzima Sebastian Maganga, alisema ushirikiano wao na Wema ni mpango mkakati wa Tatu Mzuka wa kufanya kazi bega kwa bega na Watanzania ili kuboresha maisha yao.
Maganga amesema kuwa kusudi kubwa la Tatu Mzuka kuingia makubaliano na Wema, ina lengo la kutaka kusambaza fursa kwa watu wengi kadri iwezekanavyo ili kuboresha maisha yao ya kila siku.
Kwa upande wa Wema Sepetu baada ya kusaini dili hilo amesema kuwa hana hamu kubwa ya kuanza kuwashirikisha bidhaa hii mashabiki zake wote na Watanzania kwa ujumla wao ili waweze kujitengenezea fursa nyingi za kuboresha maisha yao kupitia Tatu Mzuka.