Klabu ya soka ya West Ham United imemfuta kazi kocha wake mkuu Slaven Bilic baada ya kuwa na matokeo mabaya msimu huu.

Bilic aliteuliwa kama kocha mkuu wa West Ham majira ya kiangazi 2015 ambapo katika msimu wake wa kwanza 2015/16 aliiwezesha kushika nafasi ya saba kwenye ligi kuu ya England.

Katika msimu wake waa pili klabuni hapo 2016/17 Bilic alimaliza katika nafasi ya 11 na msimu huu ameshindwa kufanya vizuri ambapo hadi sasa timu ipo katika nafasi ya 18 ikiwa na alama 9.

Katika mechi 11 ilizocheza msimu huu wa 2017/18 timu hiyo imeshinda mechi mbili, sare tatu na kupoteza mechi 6 ikiwa imefungwa mabao 13 na kufunga mabao 7. Bilic mwenye miaka 49 amewahi kuifundisha timu ya taifa lake ya Croatia kwa miaka sita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *