Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ruby amefunguka na kusema kuwa baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu anatarajia kurudi upya mwakani.
Ruby ambaye ni zao la THT amesema kuwa amejipanga vya kutosha hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula hapo mwakani kwani atajikita kwenye kazi yake ya muziki.
Pia amesema kuwa, alikuwa kimya kwa sababu ya kujipanga na mwakani ndiyo ataanza rasmi mapambano ya kimuziki.
Amesema kuwa “Sijatoa ngoma kwa muda mrefu, lakini mwakani (2018) mashabiki wangu wategemee mambo mazuri sana, kwani ndiyo rasmi nitajikita kwenye gemu maana nilikuwa ninajipanga,”.
Kwa upande mwingine mwanamuziki huyo amekanusha kuwa na bifu na mwanamuziki mwenzake Nandy ambaye inasemakana ndiyo aliyechukua nafasi yake kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya kupotea kwenye game.